Jicho La Tatu

Bring strength, energy, motivation and initiative in the society

Range management

Tuzungumze nyanda za malisho- Tanzania

RST ANNUAL MEETING

Rangeland Society of Tanzania meeting on 27/2/2017 at Glonency 88 hotel, Morogoro

Promote land use planning in Tanzania

Avoid land users conflicts, promote development.

Jicho La Tatu

Mkombozi wa jamii.

Thursday, 19 January 2017

Leo tutizame changamoto zinazokabili wafugaji wetu hapa nchini


 Changamoto zinazokabili soko la mifugo na mazao yake.
1. —Miundombinu dhaifu kama vile masoko ya mifugo na barabara za kusafiririshia mifugo na mazao yake.
2. —Udhaifu wa mfumo wa usafirishaji wa mifugo na mazao yake.
3. —Ukosefu wa taarifa za kutosha na kuaminika za masoko ya mifugo na mazao yake ndani na nje ya nchi
4. —Udhaifu wa vyama vya wafugaji ambavyo husababisha kutopatikana kwa bidhaa nyingi za kutosheleza mahitaji ya soko.
5. Uratibu duni miongoni mwa wadau wa mnyororo wa thamani wa  mifugo.
žKutokuwa na elimu na ujuzi wa ujasiriamali. 
6. žUshindani mkubwa kutoka nchi zinazouza mifugo nje ya nchi kwa masoko yaliyopo na masoko mapya;
7. žKukosa ufahamu wa mchango na fursa za ufugaji wa asili katika mtazamo wa sekta ya mifugo nchini.
8. žUwekezaji mdogo wa serikali na sekta binafsi katika sekta ya mifugo. 
9. Uratibu duni miongoni mwa wadau wa mnyororo wa thamani wa  mifugo
10.  žKutokuwa na elimu na ujuzi wa ujasiriamali
11.  žUshindani mkubwa kutoka nchi zinazouza mifugo nje ya nchi kwa masoko yaliyopo na masoko mapya; 
12. žKukosa ufahamu wa mchango na fursa za ufugaji wa asili katika mtazamo wa sekta ya mifugo nchini. 
13. žUwekezaji mdogo wa serikali na sekta binafsi katika sekta ya mifugo. 
14. Kutotekelezwa kwa sheria ya  matumizi bora ya ardhi. Hii inatokana na kukosekana kwa mipango shirikishi ya usimamizi wa matumizi bora ya ardhi katika mchakato wa kubuni, kutekeleza na kurekebisha mipango ya matumizi ya ardhi ya kijiji. 
15. žTatizo la uhaba wa nyanda za malisho, ambalo limesababisha wafugaji kuhamahama na hivyo kufanya shughuli zao bila kuzingatia matumizi bora ya ardhi. 
16. žUkosefu wa maji hasa wakati wa kiangazi. 
17. žUshindani kutoka na mazao ya mifugo kutoka nje ya nchi ambao kwa kiasi kikubwa unachangia kukatisha tamaaa wazalishaji wa ndani.
  18. Kuwepo na milipuko ya magonjwa ya mifugo. 
19. —Ulaji duni wa mazao ya mifugo kwa watanzania ambao unadumaza soko la mifugo pamoja na mazao ya mifugo nchini. 
20. —Kutokuwepo kwa miundombinu ya usindikaji, huduma mbovu, ufungashaji wa mazao ya mifugo. 
21. —Kutopatikana kwa mikopo ya kutosha na yenye masharti nafuu kwa ufugaji ikilinganishwa na mahitaji  yao. 
22. —Uhaba wa watumishi wa nyanda za malisho katika ngazi ya Halmashauri
23Uhaba wa mbegu bora za mifugo, hii imewafanya wafugaji kuendelea kuzalisha mifugo isiyokuwa na tija. 
—ASANTENI SANA
ž
ž
 
ž

Wednesday, 18 January 2017

DHANA POTOFU KUHUSU UFUGAJI WA ASILI HAPA NCHINI HAITOTUSAIDIA.

Taifa letu limekuwa ni taifa la pili kwa wingi wa mifugo hapa barani Afrika. Jitihada nyingi zimefanywa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha wafugaji wanaendelea kunufaika katika shughuli yao ya kiuchumi. Lakini japokuwa jitihada zinafanyika bado hazijawa zenye kuridhisha na kutosheleza kulingana na mahitaji husika ya ufugaji wenyewe. Leo nijikite katika upande wa ufugaji wa asili. Ni ukweli usiopingika kwamba katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi, kijamii n.k. Na taifa letu limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaenenda sawa na mabadiliko ya ulimwengu huu. Tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya kisera na sheria mbalimbali yakifanyika ili tu kuifanya nchi yetu kuendana na mabadiliko mbalimbali ya ndani na nje ya taifa letu (jambo zuri). Lakini jambo la kujiuliza ni kweli kila badiliko fulani lazima tulikubalie (hapana). Ufugaji wa asili umedumu katika taifa kabla hata ya uwepo wa Tanzania na Tanganyika wakati ule wazee wakiishi katika mifumo yao iliyowapendeza wao kwa wakati huo. Lakini uwepo wa utaifa manake ni kukubaliana kuwa rasilimali zote ndani ya taifa hili zitumike kwa watu wote kwa usawa. Ufugaji wa asili umekuwa ni mfumo sahihi kwa wafugaji wa kitanzania kujikinga na majanga mbalimbali kama mafuriko, ukame na magonjwa mbalimbali. Wamekuwa werevu wa kutosha kuitambua ikolojia ya sehemu mbali mbali za nchi hii ili kutambua uwepo wa maji na malisho katika maeneo mbalimbali nchini. 

CHANZO CHA DHANA POTOFU.
 Kutokana na ongezeko la uhitaji wa ardhi ndio imekuwa chanzo kikuu cha dhana hii. Kutambua umuhimu wa ardhi na shughuli mbali mbali za kiuchumi zenye kufanyika ktk eneo husika yamekuwa mambo yaliyoleta dhana hii. Lakini ukweli ni kwamba ufugaji wa asili si mbaya kama watu wanavyofikiri kwa sababu ifuatayo.

UFUGAJI WA ASILI NI RAFIKI WA MAZINGIRA.
Wafugaji tangu awali wanatambua umuhimu wa utunzaji wa ikolojia ya eneo la kuchungia.Kuhama hama kwa wafugaji kumekuwa kukieleweka tofauti katika nchi yetu Watu wengi wakiamini ni kutokana na uharibifu wa eneo husika ndio maana wanahamahama lakini sio kweli, ukifatilia mfumo wao wa uhamaji utaona wafugaji huondoka eneo moja na kwenda eneo jingine kisha kurudi katika lile eneo katika msimu mwingine. Manake ni kwamba kitaalamu kuna kitu kinaitwa recovery period,unapookuwa mtaalamu wa malisho kuna muda lazma ufanye mzunguko (rotation) ya mifugo ndani ya machunga ili kuruhusu eneo lililotumika kuweza kurudi katika hali nzuri ya uzalishaji kwa ajili ya mifugo kwa wakati mwimgine. Sasa hapa ni kwamba wafugaji hutumia njia hii kiasili halafu wataalamu huleta hili jambo nji ya kisomi zaidi. Tuna sera ya mifugo ya mwaka 2006 kwa bahati mbaya nayo haijatambua na kuweka mikakati ya usimamizi na uendelezaji wa ufugaji wa asili. Tuna sera ya mazingira ambayo nayo inatambua ufugaji wa asili kama chanzo cha uharibifu wa mazingira jambo ambalo si kweli. Swala la mmomonyoko wa ardhi kutokana na ufugaji wa asili ni hoja dhaifu sana kufatana na uhalisia wa ikolojia ya maeneo husika mifano mingi imekuwa ikielekezwa DODOMA, TABORA, SHINYANGA NA SINGIDA kama mifano hai ya maeneo ambayo ardhi imeharibiwa sababu ya ufugaji kufanya overgrazing na kuzidisha uwezo wa eneo husika uwezo wake wa kuhimili idadi ya mifugo (carrying capacity). Research nyingi zilizofanyika zinaonesha hakuna uhusiano wa carrying capacity na uharibifu wa vegetation covers katika maeneo ya jangwa na nusu jangwa . Uchafuzi wa vyanzo vya maji nao si jambo la hoja ya kukandamiza ufugaji wa asili, wafugaji walitegemea vyanzo hivyo vya maji tangu awali lakini kwa vile vyanzo hivyo ni muhimu pia kwa matumizi mengine ni suala tu la kutengeneza njia mbadala ya kuwapatia maji nje ya vyanzo na kunakuwa hakuna tatizo lolote. Hatuwezi kupinga ukwelikuwa ufugaji wa asili ndio ufugaji rafiki wa nchi yetu kulingana na sababu mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kiikolojia. Ni lazima itafutwe mbinu sahihi ya kuendeleza ufugaji huu pasipo kuleta madhara, lakini matumizi ya nguvu na sheria kuukandamiza itakuwa ni chamzo cha migogoro na wafugaji wa asil wa hapa nchini.

Tuesday, 17 January 2017

UBORESHAJI NA USIMAMIZI WA MALISHO YA ASILI


Chakula kikuu anachotegemea mfugaji wa kawaida cha ng'ombe ni nyasi(grass) na majani jamii ya mikunde(legumes) ambayo haina madhara kwa afya ya mnyama kama ikitumiwa kwa usahihi.
MALISHO YA ASILI
Malisho haya (nyasi) hukua kwa uasili wa ardhi(naturally) na kupoteza viini lishe muhimu kadri yanavyozidi kukomaa(lignification na protein kushuka) . Malisho asili huwa na viini lishe vinavyotosheleza mahitaji ya mifugo kama malisho hayo yakitunzwa na kutumiwa vyema na wakati wa kiangazi malisho huwa duni (viini lishe kwa mifugo) na yasiyotosheleza. Wakati wa mvua kuna malisho yanayotosheleza na ng'ombe huwa na uzito( live body weight) na uzalishaji( production) wa kuridhisha tofauti na wakati wa kiangazi ambapo ng'ombe hupungua uzito. Malisho ya asili ya jamii ya nyasi huwa na upungufu wa viini lishe hususani protini na kuongezeka kwa lignin. Mikunde(legumes) ina tabia ya kutopungua viinilishe haraka ikilinganishwa na nyasi.
MALISHO YALIYOBORESHWA
Malisho ya asili yanaweza kuboreshwa kwa kuongeza mimea aina ya mikunde, kuongeza nyasi bora kwenye malisho, kuongeza samadi kwenye mbuga za malisho. Malisho yaliyoboreshwa yanaongeza uzalishaji wa chakula kwa mifugo na kukidhi mahitaji ya mifugo ili kufikia uzalishaji mzuri utokanao na mifugo.
TARATIBU ZA KUBORESHA MALISHO/MAMBO YA KUZINGATIA
Kuboresha malisho hakna tofauti yoyote na taratibu kama za mazao ya kawaida yalimwayo kwa ajili ya binadamu. Manake ni kwamba utafiti na teknolojia lazma itumike ili kufika lengo. Lazma uboreshaji uendane na matarajio yategemewayo kupitia mifugo.
vifuatavyo n baadhi ya vitu vya kuzingatia wakati wa uboreshaji malisho..
=>Ukubalifu kwa mifugo(acceptability)
=>Viine lishe (nutrient value)
=>Uzalishaji wa nyasi (productivity)
=>Urahisi wa uboreshaji kuepusha gharama(ease of establishment)
=>Ustahimilivu kwny magonjwa, hali ya hewa, kuchungiwa, moto n.k (persistence)
=>Uwezo wa kuchanganyika na aina nyingne ya mimea km mikunde (associative ability)
Inafaa maeneo ya kuchungia/kulishia yatengwe(gazetted) na kusimamiwa(management).
Nyasi za asili zikisimamiwa vizuri zinaweza kuongeza uzalishaji kwa mifugo pamoja na kupata chakula wakati wa kiangazi. Hii inawezekana endapo utapangwa mfumo rafk wa kuchunga kutokana na asili ya nyasi(proper grazing systems)