Tuesday, 17 January 2017
Home »
» UBORESHAJI NA USIMAMIZI WA MALISHO YA ASILI
UBORESHAJI NA USIMAMIZI WA MALISHO YA ASILI
Chakula kikuu anachotegemea mfugaji wa kawaida cha ng'ombe ni nyasi(grass) na majani jamii ya mikunde(legumes) ambayo haina madhara kwa afya ya mnyama kama ikitumiwa kwa usahihi.
MALISHO YA ASILI
Malisho haya (nyasi) hukua kwa uasili wa ardhi(naturally) na kupoteza viini lishe muhimu kadri yanavyozidi kukomaa(lignification na protein kushuka) . Malisho asili huwa na viini lishe vinavyotosheleza mahitaji ya mifugo kama malisho hayo yakitunzwa na kutumiwa vyema na wakati wa kiangazi malisho huwa duni (viini lishe kwa mifugo) na yasiyotosheleza. Wakati wa mvua kuna malisho yanayotosheleza na ng'ombe huwa na uzito( live body weight) na uzalishaji( production) wa kuridhisha tofauti na wakati wa kiangazi ambapo ng'ombe hupungua uzito. Malisho ya asili ya jamii ya nyasi huwa na upungufu wa viini lishe hususani protini na kuongezeka kwa lignin. Mikunde(legumes) ina tabia ya kutopungua viinilishe haraka ikilinganishwa na nyasi.
MALISHO YALIYOBORESHWA
Malisho ya asili yanaweza kuboreshwa kwa kuongeza mimea aina ya mikunde, kuongeza nyasi bora kwenye malisho, kuongeza samadi kwenye mbuga za malisho. Malisho yaliyoboreshwa yanaongeza uzalishaji wa chakula kwa mifugo na kukidhi mahitaji ya mifugo ili kufikia uzalishaji mzuri utokanao na mifugo.
TARATIBU ZA KUBORESHA MALISHO/MAMBO YA KUZINGATIA
Kuboresha malisho hakna tofauti yoyote na taratibu kama za mazao ya kawaida yalimwayo kwa ajili ya binadamu. Manake ni kwamba utafiti na teknolojia lazma itumike ili kufika lengo. Lazma uboreshaji uendane na matarajio yategemewayo kupitia mifugo.
vifuatavyo n baadhi ya vitu vya kuzingatia wakati wa uboreshaji malisho..
=>Ukubalifu kwa mifugo(acceptability)
=>Viine lishe (nutrient value)
=>Uzalishaji wa nyasi (productivity)
=>Urahisi wa uboreshaji kuepusha gharama(ease of establishment)
=>Ustahimilivu kwny magonjwa, hali ya hewa, kuchungiwa, moto n.k (persistence)
=>Uwezo wa kuchanganyika na aina nyingne ya mimea km mikunde (associative ability)
Inafaa maeneo ya kuchungia/kulishia yatengwe(gazetted) na kusimamiwa(management).
Nyasi za asili zikisimamiwa vizuri zinaweza kuongeza uzalishaji kwa mifugo pamoja na kupata chakula wakati wa kiangazi. Hii inawezekana endapo utapangwa mfumo rafk wa kuchunga kutokana na asili ya nyasi(proper grazing systems)






0 comments:
Post a Comment