Taifa letu limekuwa ni taifa la pili kwa wingi wa mifugo hapa barani Afrika. Jitihada nyingi zimefanywa na serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania kuhakikisha wafugaji wanaendelea kunufaika katika shughuli yao ya kiuchumi. Lakini japokuwa jitihada zinafanyika bado hazijawa zenye kuridhisha na kutosheleza kulingana na mahitaji husika ya ufugaji wenyewe.
Leo nijikite katika upande wa ufugaji wa asili. Ni ukweli usiopingika kwamba katika ulimwengu wa sasa kumekuwa na mabadiliko makubwa sana ya kiuchumi, kijamii n.k. Na taifa letu limekuwa mstari wa mbele kuhakikisha tunaenenda sawa na mabadiliko ya ulimwengu huu.
Tumeshuhudia mabadiliko makubwa ya kisera na sheria mbalimbali yakifanyika ili tu kuifanya nchi yetu kuendana na mabadiliko mbalimbali ya ndani na nje ya taifa letu (jambo zuri).
Lakini jambo la kujiuliza ni kweli kila badiliko fulani lazima tulikubalie (hapana).
Ufugaji wa asili umedumu katika taifa kabla hata ya uwepo wa Tanzania na Tanganyika wakati ule wazee wakiishi katika mifumo yao iliyowapendeza wao kwa wakati huo. Lakini uwepo wa utaifa manake ni kukubaliana kuwa rasilimali zote ndani ya taifa hili zitumike kwa watu wote kwa usawa.
Ufugaji wa asili umekuwa ni mfumo sahihi kwa wafugaji wa kitanzania kujikinga na majanga mbalimbali kama mafuriko, ukame na magonjwa mbalimbali. Wamekuwa werevu wa kutosha kuitambua ikolojia ya sehemu mbali mbali za nchi hii ili kutambua uwepo wa maji na malisho katika maeneo mbalimbali nchini.
CHANZO CHA DHANA POTOFU.
Kutokana na ongezeko la uhitaji wa ardhi ndio imekuwa chanzo kikuu cha dhana hii. Kutambua umuhimu wa ardhi na shughuli mbali mbali za kiuchumi zenye kufanyika ktk eneo husika yamekuwa mambo yaliyoleta dhana hii. Lakini ukweli ni kwamba ufugaji wa asili si mbaya kama watu wanavyofikiri kwa sababu ifuatayo.
UFUGAJI WA ASILI NI RAFIKI WA MAZINGIRA.
Wafugaji tangu awali wanatambua umuhimu wa utunzaji wa ikolojia ya eneo la kuchungia.Kuhama hama kwa wafugaji kumekuwa kukieleweka tofauti katika nchi yetu Watu wengi wakiamini ni kutokana na uharibifu wa eneo husika ndio maana wanahamahama lakini sio kweli, ukifatilia mfumo wao wa uhamaji utaona wafugaji huondoka eneo moja na kwenda eneo jingine kisha kurudi katika lile eneo katika msimu mwingine. Manake ni kwamba kitaalamu kuna kitu kinaitwa recovery period,unapookuwa mtaalamu wa malisho kuna muda lazma ufanye mzunguko (rotation) ya mifugo ndani ya machunga ili kuruhusu eneo lililotumika kuweza kurudi katika hali nzuri ya uzalishaji kwa ajili ya mifugo kwa wakati mwimgine. Sasa hapa ni kwamba wafugaji hutumia njia hii kiasili halafu wataalamu huleta hili jambo nji ya kisomi zaidi. Tuna sera ya mifugo ya mwaka 2006 kwa bahati mbaya nayo haijatambua na kuweka mikakati ya usimamizi na uendelezaji wa ufugaji wa asili. Tuna sera ya mazingira ambayo nayo inatambua ufugaji wa asili kama chanzo cha uharibifu wa mazingira jambo ambalo si kweli. Swala la mmomonyoko wa ardhi kutokana na ufugaji wa asili ni hoja dhaifu sana kufatana na uhalisia wa ikolojia ya maeneo husika mifano mingi imekuwa ikielekezwa DODOMA, TABORA, SHINYANGA NA SINGIDA kama mifano hai ya maeneo ambayo ardhi imeharibiwa sababu ya ufugaji kufanya overgrazing na kuzidisha uwezo wa eneo husika uwezo wake wa kuhimili idadi ya mifugo (carrying capacity). Research nyingi zilizofanyika zinaonesha hakuna uhusiano wa carrying capacity na uharibifu wa vegetation covers katika maeneo ya jangwa na nusu jangwa . Uchafuzi wa vyanzo vya maji nao si jambo la hoja ya kukandamiza ufugaji wa asili, wafugaji walitegemea vyanzo hivyo vya maji tangu awali lakini kwa vile vyanzo hivyo ni muhimu pia kwa matumizi mengine ni suala tu la kutengeneza njia mbadala ya kuwapatia maji nje ya vyanzo na kunakuwa hakuna tatizo lolote. Hatuwezi kupinga ukwelikuwa ufugaji wa asili ndio ufugaji rafiki wa nchi yetu kulingana na sababu mbali mbali za kiuchumi, kijamii na kiikolojia. Ni lazima itafutwe mbinu sahihi ya kuendeleza ufugaji huu pasipo kuleta madhara, lakini matumizi ya nguvu na sheria kuukandamiza itakuwa ni chamzo cha migogoro na wafugaji wa asil wa hapa nchini.







0 comments:
Post a Comment