Changamoto
zinazokabili soko la mifugo na mazao yake.
1. Miundombinu
dhaifu kama vile masoko ya mifugo na barabara za kusafiririshia mifugo na mazao
yake.
2. Udhaifu
wa mfumo wa usafirishaji wa mifugo na mazao yake.
3. Ukosefu
wa taarifa za kutosha na kuaminika za masoko ya mifugo na mazao yake ndani na
nje ya nchi
4. Udhaifu
wa vyama vya wafugaji ambavyo husababisha kutopatikana kwa bidhaa nyingi za
kutosheleza mahitaji ya soko.
5. Uratibu
duni miongoni mwa wadau wa mnyororo wa thamani wa mifugo.
Kutokuwa
na elimu na ujuzi wa ujasiriamali.
6. Ushindani
mkubwa kutoka nchi zinazouza mifugo nje ya nchi kwa masoko yaliyopo na masoko
mapya;
7. Kukosa
ufahamu wa mchango na fursa za ufugaji wa asili katika mtazamo wa sekta ya
mifugo nchini.
8. Uwekezaji
mdogo wa serikali na sekta binafsi katika sekta ya mifugo.
9. Uratibu
duni miongoni mwa wadau wa mnyororo wa thamani wa mifugo
10. Kutokuwa
na elimu na ujuzi wa ujasiriamali
11. Ushindani
mkubwa kutoka nchi zinazouza mifugo nje ya nchi kwa masoko yaliyopo na masoko
mapya;
12. Kukosa
ufahamu wa mchango na fursa za ufugaji wa asili katika mtazamo wa sekta ya
mifugo nchini.
13. Uwekezaji
mdogo wa serikali na sekta binafsi katika sekta ya mifugo.
14. Kutotekelezwa
kwa sheria ya matumizi bora ya ardhi.
Hii inatokana na kukosekana kwa mipango shirikishi ya usimamizi wa matumizi
bora ya ardhi katika mchakato wa kubuni, kutekeleza na kurekebisha mipango ya
matumizi ya ardhi ya kijiji.
15. Tatizo la
uhaba wa nyanda za malisho, ambalo limesababisha wafugaji kuhamahama na hivyo
kufanya shughuli zao bila kuzingatia matumizi bora ya ardhi.
16. Ukosefu
wa maji hasa wakati wa kiangazi.
17. Ushindani
kutoka na mazao ya
mifugo kutoka nje ya nchi ambao kwa kiasi kikubwa unachangia kukatisha tamaaa
wazalishaji wa ndani.
18. Kuwepo na
milipuko ya magonjwa ya mifugo.
19. Ulaji
duni wa mazao ya mifugo kwa watanzania ambao unadumaza soko la mifugo pamoja na
mazao ya mifugo nchini.
20. Kutokuwepo
kwa miundombinu ya usindikaji, huduma mbovu, ufungashaji wa mazao ya mifugo.
21. Kutopatikana
kwa mikopo ya kutosha na yenye masharti nafuu kwa ufugaji ikilinganishwa na
mahitaji yao.
22. Uhaba wa
watumishi wa nyanda za malisho katika ngazi ya Halmashauri
23Uhaba wa
mbegu bora za mifugo, hii imewafanya wafugaji kuendelea kuzalisha mifugo isiyokuwa na tija.
ASANTENI SANA






0 comments:
Post a Comment